Mkazi wa kijiji cha Ihebo Kata ya Muriti wilayani hapa Mkoa
wa Mwanza, Ese Benaya (19) anadaiwa kumlawiti mdogo wake mwenye umri wa miaka
miwili (mtoto wa baba yake mkubwa) na kumsababishia maumivu makali.
Akizungumza leo Julai
26, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema tukio hilo lilitokea
Julai 25 saa sita mchana kijijini hapo
Kamanda Msangi amesema mtoto huyo alikuwa akicheza na watoto
wenzake kwenye nyumba anayoishi mtuhumiwa na hivyo mtuhumiwa huyo alitumia
fursa hiyo kuwatuma watoto wenzake dukani kununua sindano ya kushona nguo
Kwa mujibu wa Msangi, mtuhumiwa alimchukua mtoto huyo na
kumuingiza ndani kisha kumlawiti na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za
siri
“Baada ya mtuhumiwa kufanya kitendo hicho cha kikatili
alitoroka na kukimbilia kusipojulikana akimuacha mtoto anapiga kelele za kuomba
msaada ndipo mama wa mtoto alifika akamkuta mtoto ana hali mbaya na kutoa
taarifa polisi,” amesema
Kamanda Msangi amesema wakati polisi ikiendelea kumsaka
mtuhumiwa ili sheria ichukue mkondo wake, mtoto amelazwa katika hospitali ya
wilaya ya Ukerewe akiendelea na matibabu na kwamba afya yake inaendelea
kuimarika
Adaiwa kumlawiti mdogo wake wa miaka miwili
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment