Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi (TSN) na Mwanafunzi wa
mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo amekamatwa na
jeshi la polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuonekana katika maeneo ya chuo
hicho
Akizungumza kwa njia ya simu leo Julai 27, 2018 wakili wa
mwanafunzi huyo Jebra Kambole amesema Nondo alikamatwa Julai 26 saa tatu usiku
wakati akizungumza na wenzake, katika eneo la chuo hicho
Inaelezwa kuwa Nondo alikwenda kuchukua vitu
vyake chuoni hapo
Kambole amesema wakati Nondo anaondoka chuoni hapo aliacha baadhi
ya vitu ambavyo alilazimika kuvifuata baada ya wenzake kufunga chuo
“Alikutana na wenzake chuoni hapo wakawa wanajadiliana
baadhi ya mambo ndipo askari wa eneo la chuo walimkamata na kumuweka ndani,”
amesema Kambole na kuongeza:
“Lakini eneo alilokamwatwa ni ambalo mtu yeyote anaweza
kupita kwa sababu hata magari ya kwenda Mwenge yanapita.”
Amesema kwa mujibu wa maelezo ya awali aliyopewa ni kuwa
Nondo amekamatwa kwa kosa la kuingia eneo la chuo kinyume cha sheria
“Lakini katika barua ya kusimamishwa chuo aliyopewa hakuna
sehemu iliyoandikwa kuwa hatakiwi kufika eneo la chuo sasa kwanini akamatwe,”
amesema Kambole
Amesema tayari wameshaandaa wadhamini na wanasubiri tu
maelezo
Abdul Nondo akamatwa kwa ‘kutia’ mguu UDSM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment