Watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana wamelazwa katika
chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo leo
Julai 27 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dk Abel Makubi amesema watoto
hao wa kiume walizaliwa kwa njia ya upasuaji na wataalamu wa afya wameona
wanahitaji uangalizi maalumu
Dk Makubi alikuwa akimtembeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
John Mongella aliyekwenda kuwaona pacha hao
Kwa mujibu wa Dk
Makubi watoto hao wamezaliwa na Angelina Ramadhani (34) mkazi wa Nyakato jijini
Mwanza, wameungana sehemu ya kifua na tumbo
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo mama wa watoto hao anaendelea
vizuri
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kulingana na
taratibu za kitabibu haikuwezekana kuwaona watoto hao badala yake taarifa
zitakuwa zikitolewa na wataalamu kulingana na maendeleo yao
“Niombe tu, kuna taarifa zimeshasambazwa kwenye mitandao
ambazo zinapotosha jambo hili, watoto nimewaona kwa macho wanaendelea vizuri
hata mimi nilidhani tungeweza kuwaona sote lakini kila kitu kina miiko na
taratibu zake,” amesema Mongella
Pacha walioungana walazwa ICU Bugando
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment