Baada ya kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Lazaro Mambosasa kusema askari waliotuhumiwa kumuua kwa risasi aliyekuwa
mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini
wameachiwa huru, familia ya binti huyo imeitaka Serikali iwaambie ni akina nani
walihusika na mauaji hayo
Richard Akwilini, kaka wa Akwilina akizungumza na Mwananchi
jana, alisema kwa kuwa jukumu lote kuhusu tukio la kuuawa mwanafunzi huyo
lilibebwa na Serikali wanataka kusikia tamko kutoka kwao ni nani alihusika
“Tumesikia kwenye vyombo vya habari askari waliotuhumiwa
kumuua ndugu yetu wameachia huru, ni sawa. Lakini familia tunataka kujua ni
nani aliyekuwa amebeba silaha iliyomuua ndugu yetu?” alihoji Richard
Dismas Shirima, msemaji wa familia ya Akwilini alisema
wakati wa tukio la mauaji Rais John Magufuli alieleza kusikitishwa na kitendo
hicho, hivyo wanasubiri tamko na busara kutoka kwake kwa sababu Serikali
ilibeba jukumu la suala hilo
“Tunaamini baada ya askari kuachiwa Rais Magufuli atasema
jambo na tunajua atatenda haki ili kujua ukweli uko wapi. Tunachosubiri kutoka
kwake ni busara zake kama Rais wa wanyonge ili jambo hili litendewe haki,”
alisema Shirima.
Akwilina aliuawa kwa
kupigwa risasi Februari 16, akiwa kwenye daladala eneo la Kinondoni Mkwajuni
jijini Dar es Salaam akitokea Mabibo wakati askari wakiwatawanya wafuasi wa
Chadema waliokuwa wakielekea ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
Kinondoni
Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne wiki hii, Kamanda
Mambosasa alisema askari waliokuwa wanashikiliwa kutokana na tukio za mauaji ya
mwanafunzi huyo waliachiwa baada ya ushahidi kuwa hafifu
Akielezea tukio hilo, kamanda huyo aliwatuhumu Chadema kwa
kuhamasisha maandamano ya kisiasa yaliyofanyika Februari 16, siku moja kabla ya
uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni
Kauli hiyo ilijibiwa na mwenyekiti wa Baraza la Vijana
Chadema (Bavicha), Patrick ole Sosopi aliyesema inalenga kuwaaminisha wananchi
kuwa shughuli za chama chao ni hatari na si salama kwa watu kuhudhuria
Familia yataka Serikali kueleza nani alimuua Akwilina
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment