Mzee wa miaka 71 akutwa na Nyaraka Bandia Za Serikali


JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mzee wa miaka 71 na watu  wengine watatu baada ya kukutwa na Nyaraka  bandia za serikali 240  ambazo wamekua wakiziandaa kwa njia ya udanganyifu pamoja na Mihuri 159 na kuuzwa kwa bei ya Sh 20,000

Nyaraka zilizo kamatwa ni pamoja na Vyeti vya kuzaliwa ,vyeti vya ndoa ,vyeti vya ubatizo,vyeti vya  Kliniki na matamko ya vizazi na vifo pamoja na mihuri mbalimbali miongoni mwao ikionyesha ni ile inayotumika wakati wa usajili vizazi na
vifo katika manispaa ya Moshi na Kitete mkoani Tabora.<

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa  alisema vifaa vingine vilivyo kamatwa ni pamoja na Mashine moja ya  kuandikia (Type Writer) na kifaa cha kuwekea namba huku akiwataja  watuhumiwa kuwa ni pamoja na Athuman Selemani (71) anayetajwa kuwa  aliwahi kuwa mtumishi wa serikali katika ofisi ya mkuu wa wilaya

Wengine ni Justine Mziray (55) anayetajwa kuwa ni mtaalamu wa kuchonga mihuri,Sporah Daud anayetajwa kushiriki katika uandaaji wa nyaraka hizo  kwa kuchapa maandishi kwa kutumia mashine maalumu (Type writer) na Costa Lyatuu anayetajw kuwa mtaalamu wa kughushi sahihi
Mzee wa miaka 71 akutwa na Nyaraka Bandia Za Serikali Mzee wa miaka 71 akutwa na Nyaraka Bandia  Za Serikali Reviewed by KUSAGANEWS on July 24, 2018 Rating: 5

No comments: