SHILOLE AAMUA KUSOMA KIINGEREZA KWA WATAALAMU WA LUGHA DUNIANI

Baada ya kuchekwa sana kwa kutojua kiingereza, msanii wa bongo flava Shilole ameingia mkataba na shirika la Uingereza British Council Tanzania ili kujifunza lugha hiyo

Mbali ya muziki, msanii huyo anajulikana sana kwa kuwa na hamasa ya kuongea kiingereza bila kujali makosa ambayo anayafanya. Wiki iliyopita tuliona video ikitrend ya mwanadada huyo akijaribu kusema   alivyokua anaongelea kuhusu wimbo wake mpya

Shirika la Uingereza British Council Tanzania, limefurahi Shilole ameamua kutaka kujiendeleza katika lugha ya kiingereza ambayo itamsaidia katika kazi yake kama msanii

Hususani kumpa fursa za kimataifa zaidi. Angela Hennelly, Country Director, amesema kuwa ni fursa nzuri kwa Shilole kujua lugha ya Kiingereza na amempongeza kwa hatua hiyo aliyoichukua. 

Ameendelea kusema kuwa hii itamfungulia milango mingi ya fursa kulingana na jinsi uchumi wa dunia unavyokua na changamoto wanazozipata haswa wasanii

Angela ameendelea kusema kuwa anategemea hii fursa itawapa moyo vijana kufikiria pia kujiendeleza katika lugha ili waweze kufanya mawasiliano kwa urahisi katika shughuli zao za kila siku haswa kwa upande wa ajira

SHILOLE AAMUA KUSOMA KIINGEREZA KWA WATAALAMU WA LUGHA DUNIANI SHILOLE AAMUA KUSOMA KIINGEREZA KWA WATAALAMU WA LUGHA DUNIANI Reviewed by KUSAGANEWS on July 24, 2018 Rating: 5

No comments: