Wakati aliyekuwa waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba
akiibukia wilayani Babati mkoani Manyara kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya
Bagara (CCM), Nicodemus Tlaghasi, mgombea ubunge wa Chadema katika Jimbo la
Buyungu, Eliya Michael anavuta subira kuanza kampeni
Michael anayechuana na Christopher Chiza wa CCM katika
uchaguzi huo unaofanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago
kufariki dunia Mei 26, alisema hoja yake kubwa itakuwa kuimarisha ulinzi
shirikishi kutokana na kuibuka kwa matukio ya utekaji na uhalifu
Katika kampeni zilizofanyika juzi jioni kwenye viwanja vya
Mtaa wa Mji Mpya mjini Babati, Mwigulu alikuwa pamoja na mbunge wa Babati
Vijijini (CCM), Jitu Vrajlal Soni
Mwigulu aliwaomba wakazi wa eneo hilo kumchagua Tlaghasi ili
kumuunga mkono Rais John Magufuli katika juhudi zake za kufanikisha maendeleo
ya wananchi, hasa miradi mikubwa anayoianzisha nchini.
“Maendeleo yote
yanayofanyika nchini ni utekelezaji wa ilani ya CCM, hivyo msipotoshwe na
wapinzani hapa Babati wanaojinadi kuwa watatekeleza mambo ya maendeleo, hizi
barabara za lami na miradi ya maji ni kazi ya Rais Magufuli,” alisema.
Alisema wananchi wa
kata hiyo hawana sababu ya kupoteza muda kumchagua mgombea udiwani ambaye
hatokani na CCM kwa sababu hawezi kuwa daraja la kuwapeleka kwenye maendeleo
Naye Jituson alisema wananchi wa Kata ya Bagara walifanya
kosa siku za nyuma, hivyo wasirudie tena kosa hilo kwa kumchagua mgombea wa
upinzani
“Tlaghasi aliona mbali kwa kujitoa Chadema na kujiunga na
CCM, hivyo huu ndiyo wakati wa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kumchagua
mgombea wa CCM kwenye ngazi ya udiwani,” alisema Jituson
Tlaghasi aliwaomba wananchi wa Bagara wampe kura za kishindo
ili aweze kuendelea kuwatumikia akiwa kwenye chama tawala
Mgombea huyo alijiuzulu udiwani akiwa Chadema na kujiunga na
CCM ambayo imempitisha kuwania tena nafasi hiyo
Ulinzi wawatesa Chadema
Kwa upande wake, Michael anayegombea Jimbo la Buyungu kwa
tiketi ya Chadema, alisema matukio ya utekaji yamesababisha athari nyingi
katika shughuli za kiuchumi na kuwafanya wananchi kuishi maisha ya hofu
Eliya, ambaye ni diwani wa Kata ya Gwarama, alisema tangu
alipochaguliwa mwaka 2015, vifo 36 vimetokea katika kata hiyo vikihusiana na
matukio hayo ya utekaji nyara na uhalifu mwingine
“Baada ya kuona takwimu hiyo nilihamasisha watu wa Kata ya
Gwarama kufanya ulinzi shirikishi na kuweka zamu ya doria, tangu kipindi hicho
hakujatokea tukio lolote kwenye kata hii,” alisema
“Wananchi wengi wanaamini kuwa jukumu la ulinzi ni la
polisi, lakini wanasahau kwamba polisi wetu ni wachache, hivyo lazima
tushirikiane kulinda mipaka na maeneo yetu ya makazi,” alisema
Kuhusu kuchelewa kuanza kampeni, Eliya ambaye ni diwani
kupitia Chadema, alisema ilitokana na msimamizi wa uchaguzi kuchelewa
kuunganisha ratiba za vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo
Aomba kura kwa kupiga magoti
Wilayani Kyela mkoani Mbeya mgombea udiwani wa Kata ya
Mwanganyanga (Chadema), Alfredy Andembwise alilazimika kupiga magoti kuwaomba
wananchi kumchagua, huku akieleza vipaumbele vyake vitatu
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa kampeni
zake juzi jioni kwenye viwanja vya Mtaa wa Mkombozi, Andembwise alivitaja
vipaumbele vyake kuwa ni kuendeleza miradi ya kuunganisha barabara za mitaa,
kuhamasisha wananchi kupata kituo cha afya na kufungua akaunti maalumu ya kata
kwa ajili ya kusaidia vijana na wanawake
Nyongeza na Godfrey Kahango
Mwigulu amnadi mgombea udiwani Babati
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment