KATIKA kuelekea iliko uchumi wa Tanzania ya Viwanda nchini,
wilaya ya Mkuranga iko mbele na imeitikia wito huo ikiwa na kasi kubwa ya
kukaribisha wawekezaji wengi
Pia, ni mahali inakopita Barabara ya Kilwa, kuelekea mikoa
ya Kusini mwa nchi ambako mtu akipita, haijifichi kuonekana mwitikio wa
uwekezaji mkubwa barabarani, viwanda vinavyotengeneza malighafi mbalimbali
Ni siku chache zilizopita akiwa mkoani Pwani katika kuweka
jiwe la msingi wa ujenzi wa Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John
Magufuli, alirejea ukweli kuwa Pwani ndio kinara kitaifa kuwa na viwanda vingi
vipya.
Hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Injinia Everist
Ndikilo, alipokea Mwenge wa Uhuru ukitokea jijini Dar es Salama, akikabidhiwa
na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Injinia Ndikilo, anasema mkoa wa Pwani
pamoja na kuwa na wilaya saba, anapaeleza Mkuranga
pamebarikiwa kuwa na viwanda vingi
Anasema kutokana na Tanzania kuwa ya Viwanda, kuna jumla ya
vijana 2000 kutoka mkoa wa Pwani, waliopatiwa mafunzo ya kujiandaa kufanya kazi
viwandani
Kwa mujibu wa Injinia Ndikilo, asilimia 20 ya wafanyakazi
viwanda wanaishi ndani ya mkoa huo, huku kukifanikiwa kuwa na kiwanda cha kuua
wadudu kinachotengeneza dawa za kutibu ugonjwa wa malaria
Injinia Ndikilo, aliyekuwa akisoma risala kwa mkimbiza
mwenge kitaifa, Charles Kabeho, mara baada ya kuupokea mwenge katika viwanja
vya Shule ya Msingi Kiparampakani, Mkuranga anasema kuwa miradi ya maendeleo
yenye zaidi ya thamani ya Sh. bilioni 162, itazinduliwa katika mkoani humo
Ndikilo anasema; "Miradi hiyo inatekelezwa na nguvu za
wananchi, serikali kuu na wadau wa maendeleo."
Huku akirejea kaulimbiu ya mwenge kitaifa mwaka huu “Mpatie
Mwanao Elimu, kwani Elimu ni Ufunguo wa Maisha,’ anafafanua hali ya uandikishaji
wanafunzi imeongezeka kutoka watoto 56,000 mwaka 2017 hadi kufikia watoto zaidi
ya 300,000 mwaka huu. Ni ongezeko kwa wastani wa zaidi ya asilimia 500
Mkuu wa Mkoa anasema, wamekuwa wakiwajengea uwezo wanafunzi
kupenda masomo ya sayansi, kwa lengo la kufanikisha ongezeko la wataalamu wa
sayansi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbeto Sanga, anasema kuna
miradi tisa yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 2.6 imezinduliwa Mkuranga na
kiongozi wa Mbio za Mwenge
Anasema katika kutekeleza safari kuelekea Tanzania ya
Viwanda, Mkuranga imefanikiwa kupata wawekezaji wengi katika sekta ya viwanda
Pia, katika kufikia malengo ya kuwapata wataalamu
kitaifa, shule zimekuwa zikihamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi,
lengo ni kupata wataalamu katika soko la viwanda
Kwa mujibu wa Ofisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya
Mkuranga, Michael Mpupua, wilaya ina viwanda 58 vinavyofanya kazi hadi sasa na kuna
viwanda vitano vilivyopo katika hatua ya kujengwa
Ofisa Elimu ya Msingi, anaeleza kuwa Mkuranga ina shule za
msingi 126, 113 za serikali na 33 binafsi
Anasema mwaka huu, kuna wanafunzi 5346 waliandikishwa
kujiunga na elimu ya awali, huku elimu ya msingi ikivunja rekodi baada ya
wanafunzi 12,443 kuandikishwa kujiunga na darasa la kwanza
Kabeho ambaye ni Mkimbiza Mwenge Kitaifa, anaipongeza
Mkuranga, kwa kufanikiwa kuwa na wawekezaji wengi
Hata hivyo, anakumbusha kwamba ili kufanikiwe kuwa na
Tanzania ya Viwanda, kuna kila sababu ya kuwahamasisha wanafunzi kujikita
katika masomo ya sayansi, lengo ni kufanikisha upatikanaji wataalamu bora
Pia, kutokana na kaulimbiu ya mwenge kitaifa
inayohimiza elimu, Kabeho anahimiza: "Urithi wa mtoto ni elimu,
hivyo ni wajibu kwenu wazazi kuhakikisha elimu mnawapatia watoto kwenu,"
anasema
Pia, anahimiza miradi ya maendeleo inapaswa kusimamiwa kwa
wakati na fedha za miradi zinazotolewa zinapaswa kuendana na miradi halisi
Kabeho anasema kuna baadhi ya halmashauri zinazoshindwa
kusimamia miradi yake ya maendeleo, hata ikashindwa kukamilika kwa wakati
lewa na serikali na wadau wa maendeleo, lakini baadhi ya
watu sio wa kweli katika kusimamia miradi hiyo,” anasema Kabeho
Anawataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi, ili
kuwaletea maendeleo wananchi wao, kwani wapo baadhi ambao utendaji wao huendani
na kasi ya kiongozi wa nchi, Rais Dk. John Magufuli, ambaye amekuwa akiwataka
watendaji hao kutatua kero za wananchi
Kwa mujibu wa Kabeho, Mkuranga ni wilaya ya 121 katika
mzunguko wa kukimbiza mwenge
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliyeukabidhi
mwenge Mkuranga, anasema mkoa wake umezindua miradi yenye thamani ya Sh.
bilioni 32
Akisoma taarifa ya Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda anasema
kuna miradi miwili yenye thamani ya Sh. milioni 500, ambayo
haikupitiwa na Mwenge wa Uhuru, kwa sababu ya kukosa vigezo stahiki
Makonda anasema kutokana na kaulimbiu ya mwenge,
inayozungumzia elimu, rushwa na dawa za kulevya, Dar es Salaam, iko mstari wa
mbele kupambana na athari ya dawa za kulevya
Anasema jamii imekuwa ikihamasika na kutoa taarifa kwa watu
wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya, kwamba kuna vijana kati ya 900
hadi 1000 walioko katika vituo vya ushauri nasaha na kati yao, vijana vijana
300 wameshaanza kupata dawa
Hiyo pia ina athari zake, ikiwa ni nguvu kazi muhimu
inayohitajika katika gurudumu la maendeleo kuelekea Tanzania ya Viwanda
Kuhusu
rushwa mkoani kwake, Makonda anasema mapambano yanaendelea na ni jambo
linalochangia kurudisha nyuma maendeleo
Mwenge watua mkuranga ukikutana na viwanda 56 vinavyofanya kazi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment