Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema hakuna
utoroshaji wa madini ya Tanzanite uliofanyika hadi kusababisha kushuka kwa
malipo ya mrabaha kutoka Sh444 milioni hadi Sh40 milioni kwa mwezi
Amesema hali hiyo inatokana na uzalishaji mdogo wa madini
hayo migodini na kusababisha mapato kushuka
Mnyeti amesema hayo leo Julai 22, 2018 wakati akizungumzia
na Mwananchi kuhusu taarifa iliyotolewa hivi karibuni kuwa mapato ya
mrabaha kwa sababu ya utoroshaji
Amesema mapato hayajashuka sababu ya madini kutoroshwa ila
mapato yameshuka baada ya uzalishaji kuwa duni kwenye kipindi cha miezi mitatu
iliyopita katika migodi ya madini ya Tanzanite
"Kuanzia Aprili, Mei na Juni hakukuwa na uzalishaji
mkubwa ila ilikuwa ni kwenye mgodi mmoja wa kampuni ya Iraqw mining ndiyo
ulizalisha kwa kiasi kikubwa zaidi ya migodi yote," amesema Mnyeti
Amesema mrabaha ungepatikana mkubwa kutokana na migodi hiyo
kuzalisha madini mengi lakini siyo sahihi ukisema utoroshaji umefanyika ili
hali ni mgodi mmoja pekee wa Iraqw mining uliozalisha kwa wingi
"Kuna uchimbaji na uzalishaji, hivyo hivi sasa ni
kipindi cha uchimbaji na wameanza kuzalisha kwenye baadhi ya migodi hivyo mwezi
wa nane kutakuwa na mapato mengi yatakayotokana na mrabaha utakaolipwa
serikalini," amesema Mnyeti
Mnyeti atoa neno kushuka mapato ya Tanzanite
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment