Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla
amewaomba wanasiasa wenzake, kufanyakazi ya kumsaidia Rais John Magufuli,
kudhibiti mifugo kuingia hifadhini badala ya kutetea uvamizi huo
Akizungumza na waandishi wa habari, katika eneo la hifadhi
ya jamii ya Makao, Dk Kigwangalla amesema changamoto katika uhifadhi kwa
sasa ni mifugo, hivyo yeye na wanasiasa na viongozi wa Serikali waliochaguliwa
wanapaswa kusimamia sheria za nchi kutokana na nafasi zao walizoteuliwa
kumsaidia Rais Magufuli
Amesema maeneo mengi ya hifadhi yamevamia kuna watu
wanajenga hadi katika ndani ya eneo la mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na hao
mara nyingi ndio wanaingiza mifugo hifadhini usiku na kufanya ujangili
Waziri huyo, pia alitembelea kambi ya kitalii ya TGTS na
hoteli ya Mwiba na kushuhudia vikosi vya kupambana na ujangili katika maeneo hayo
ambavyo vipo hapo chini ya Taasisi Friedkin Conservation Fund na kueleza
kuridhishwa na uwekezaji wa taasisi hiyo
Mkurugenzi wa Mwiba Holding, Abdukaril Mohamed, amesema
katika eneo la Mwiba wamewekeza Sh2.2 bilioni na hivi sasa wanaendelea na
shughuli za uhifadhi na utalii
"Mheshimiwa Waziri (Kigwangalla) katika eneo hili,
kampuni yetu inafanya utalii wa picha na kuna hoteli, tunafanyakazi kwa amani
na utulivu na vijijini vinavyotuzunguka," amesema
Mwenyekiti wa kijiji cha makao, Anthony Philip, alimweleza
Waziri Kigwangalla kuwa, katika eneo hilo kuna mahusiano mazuri baina ya vijiji
na wawekezaji na vijiji vinapata mgao wa fedha
Amesema kijiji cha makao kimekuwa kikipata zaidi ya Sh147
milioni kwa mwaka kutoka kwa mwekezaji na vijiji vingine sita vimekuwa vikipata
zaidi ya Sh80,000 milioni kila mwaka
Akiwa katika pori la akiba la Maswa, Meneja wa pori hilo,
Lusato Masinde amesema wanauhusiano mzuri na wawekezaji ambao licha ya kulipia
ada za vitalu pia wamekuwa wakitoa msaada wa huduma mbalimbali ikiwepo maji
Hata hivyo, amesema katika pori hilo changamoto kubwa ni
uvamizi wa mifugo, uchache wa watumishi na upungufu wa vitendea kazi
Kigwangalla awaomba wanasiasa kufanyakazi za kumsaidia Rais kudhibiti mifugo hifadhini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment