Mbunge wa jimbo la Longido mkoani Arusha Dkt Steven
Kiruswa amempongeza Mbunge mtaafu Bwana Lekule Laizer ambaye aliongoza jimbo
hilo kwa miaka 20 na kumuahidi kuwa yale yote mema aliyoyanzisha katika kipindi
cha uongozi wake atayaendeleza.
Dkt Kiruswa ameyasema hayo katika sherehe ya kustaafu
kwa Mh Lekule ambapo zilifanyika nyumbani kwake Mundarara ambapo walishiriki
viongozi wa kitaifa akiwemo naibu waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Mh
William Olenasha , Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka ,mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Arusha Loata Sanare ,Viongozi wa wilaya na kata pamoja na wananchi.
Mbunge Dkt Kiruswa amesema kitendo kilichofanyika siyo
sherehe tu bali ni kama tuzo ya kumpongeza Mh Lekule kwa kazi nzuri aliyofanya
wakati akiwa Mbunge wa jimbo hilo ambapo kuna mengi aliyoyafanya ikiwemo
kutetea ardhi ya wananchi wa Longido.
Amesema kati ya mambo ambayo ataendeleza ni pamoja na ulinzi
ardhi kwa kuwa moja ya migogoro iliyokuwemo kipindi cha nyuma ni wananchi kupambania
ardhi hivyo atahakikisha anaendelea
kulinda na kusimamia ardhi ya Longido.
Pamoja na hayo Dkt Kirushwa ameongeza kuwa vile vile
atahakikisha anasimamia masuala ya upatikanaji wa maji kwa wananchi kwa kipindi
chote ambapo miradi mbalimbali inaendelea kuboreshwa zaidi ambapo Mh Lekule
alianzisha kupambania huduma ya upatikanaji wa maji.
Kwa upande wa elimu amesema pia atahakikisha
anahamasisha jamii za kifugaji kupeleka watoto shule kwa kuwa Lekule aliboresha
upatikanaji wa elimu pia ameahidi kuendeleza jambo ili wilaya hiyo ya Longido
iwe na wasomi zaidi.
Amesisitiza kuwa upo mfuko ambao mbunge huyo Mstaafu
mzee Lekule alianzisha kwa ajili ya watoto kwenda shule za msingi na sekondari amesema
yeye ataboresha zaidi ili watoto wafike Vyuo vikuu ili wapatikane wataalamu wa Masomo ya Sayansi,Madaktari pamoja na
wataalamu wa fani mbalimbali.
Hata hivyo Kiruswa amesema yuko tayari kutumikia
wananchi wake kwa nguvu zote na wandelee kumtuma kwasababu tayari wamempa
ridhaa ya kuwatumikia kama Mbunge wao.
Awali akitoa wosia Mbunge Mstaafu Mh Lekule amesema hana
wasiwasi na Dkt Kiruswa kwa kuwa ni Mbunge msikivu na hana majivuno anajali
wananchi wake na kuahidi kumpa ushirikiano wowote atakaotaka kutoka kwake.
Mzee Lekule pia amemtaka Kiruswa kukumbuka kuwa kwenye
uongozi kuna changamoto nyingi ambazo zina katisha tama lakini aendelee
kuvumilia kwasababu anaweza kuongoza ndiyo mana akapewa dhamana hiyo ya
kuongoza wananchi bila kujali itikadi zao za vyama.
Sherehe hizo zimehudhiriwa na wananchi zaidi ya 1000
ambapo walimpongeza Lekule kwa kuwa amewaletea maendeleo ,ikiwemo Elimu ,Afya
pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi ambayo iliwakosesha amani kwa muda mrefu
bila kupata msaada.
Mzee Lekule amewahi kuwa kiongozi kuanzia ngazi ya kijiji
na mpaka alipostaafu alikuwa mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha.
Mbunge wa Longido Dkt Steven Kiruswa Amuahidi mambo muhimu Mbunge Mstaafu Lekule Laizer
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment