Waziri wa
Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ametaka raia wa Msumbiji waliokimbilia Tanzania,
warudishwe nchini kwao ndani ya siku tatusema hali ya usalama nchini shwari,
yakiwemo maeneo wanayoishi raia wa Msumbiji waliokimbia uhalifu nchini kwao
Julai mwaka
jana, zaidi ya Watanzania 600 waliokuwa wakiishi Msumbiji na baadhi ya raia wan
chi hiyo jirani, walivuka mpaka wa Mto Ruvuma na kuingia Tanzania baada ya
kutokea vurugu katika Kijiji cha Kisungure.
Baada ya uhakiki, ilibainika kuwa kati yao,
watanzania walikuwa 544 na wengine 92 walikuwa rais wa Msumbiji na mustakabali
wa kurejeshwa kwao ulikuwa ukisubiri mazungumzo baina ya serikali za nchi hizi
mbili
Lakini jana,
Waziri Lugola alisema hali sasa ni shwari nchini Msumbiji na kuagiza warejeshwe
kwao ndani ya siku tatu
"Isituchukue
muda zaidi ya siku tatu tukiwa bado tunahangaika na kikundi cha watu wasiozidi
200 hapa kurudishwa Msumbiji,” amesema waziri huyo ambaye ameanza kasi kwa
kishindo baada ya kuteuliwa mapema mwezi huu
“Warudi (kwao)
waendelee na shughili zao. Hatuwezi kuendelea kuwaweka ilhali sisi hatuna kambi
ya wakimbizi hapa."
Lugola amesema
hayo wakati alipotembelea eneo wanakoishi raia hao wa Msumbiji wapatao 102
katika kijiji cha Kivava wilayani Mtwara.
Waziri Luoga amewaambia watu hao kuwa hawana
hadhi ya ukimbizi kwa kuwa Msumbiji hakuna machafuko ya kisiasa, bali ni baadhi
ya wahalifu waliofanya matukio yaliyosababisha wakimbie nchi
"Nimezungumza
nao na wamesema wako tayari kurudi nchini kwao kuendelea na maisha yao. Na mimi
nakubaliana nao na ndio maana sasa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa tayari wamejipanga vizuri na sisi vyombo vya usalama
na serikali ya mkoa tumejipanga kuhakikisha wanarudi," amesema Kugola
Aidha
ameiagiza uongozi wa mkoa kuhakikisha wanawaangalia kwa makini
Watanzanaia wanaorudi kutoka Msumbiji, akisema baadhi yao walienda kinyemela na
hivyo Idara ya Uhamiaji haina kumbukumbu zao
"Watanzania
wa namna hiyo lazima tuwaangalie kwa umakini, na katika kuwaangalia hatuwezi
tukatumia fedha ambazo Mheshimiwa Rais anahangaika kila siku kuzikusanya maeneo
mbalimbali,” amesema
“Badala ya
kuzielekeza kwenye huduma halafu aanze kuzielekeza kwa wenzetu ambao wanatoka
nchini kinyemela halafu yanapowakuta kule tuanze kuwalisha na kuwasafirisha?
Mheshimiwa mkuu wa mkoa, katika Serikali hii hilo halina nafasi hakuna kumlisha
mtu wa aina hii."
Alisema kundi
la pili ni Watanzania waliokwenda Msumbiji kihalali ambao ametaka
waangaliwe vizuri kwa kuwa wanaweza pia wahalifu
“Wapigwe tochi
vizuri. Unaweza kuwa umeenda kuhalali lakini bado ni muhalifu. Na wao
mkishawapitia vizuri basi waweze kurejea katika maeneo yao," amesema
Lugola
Alitaka vyombo
anavyovisimamia kuendelea kufanya shughuli zao katika maeneo wanayoishi raia wa
Msumbiji ili kuwabana wahalifu waliokimbia
"Sisi
tunajua kuna watu ambao tunawatafua wanafanya uhalifu maeneo yetu haya (halafu)
wamekimbilia Msumbiji,” amesema Lugol
“Sasa wasije wakatumia fursa hii kurudi huku
ndani. Lazima tukabe maeneo haya, lazima. Hakuna penati itakayopigwa bila
kukabwa na anayesimamia chombo chochote kilicho chini yangu, ikitokea hawa
ambao wanataka kutumia mwanya wakurudi na badaye ikabainika ni wahalifu na
hawakuwachuja vizuri, basi huyo anayesimamia chombo hicho atapata tabu sana
“Atapata msukosuko
yeye huyo ambaye hakusimamia eneo lake vizuri; iwe ni Jeshi la Polisi,
Uhamiaji, Magereza, Zimamoto au vitambukisho watapata tabu sana."
Mmoja wa raia
waliozungumza mbele ya waziri, Suzan Kolimba ameomba kurejeshwa nchini kwao ili
kuendelea na shughuli zao
Naye Waziri
Kolimba amesema wao kama wizara wana wajibu wa kujenga mahusiano mazuri baina
ya Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji ambayo pia ni nchi marafiki
"Inapotokea
kanzia yoyote ambayo inagusa raia wa kwetu ambao wako kwenye nchi nyingine,
sisi kama wizara huwa tunashughulikia hilo jambo kwa karibu zaidi kuhakikisha
tunatatua kadhia na changamoto,” alisema Kolimba
“Ndio maana
mnaona niko hapa, lakini pia tuna maafisa wetu wako Msumbiji ili kuhakikisha
raia walio Msumbiji kwenye maeneo ambayo kadhia hii imetokea, wanashughilikiwa
na kutatuliwa matatizo ambayo yapo,"amesema Kolimba
Raia hao
walianza kuingia nchini wakitoka nchini Msumbiji kwa madai ya uwepo wa vurugu
ambapo watanzania idadi yao ilikuwa 544 na raia wa Msumbiji walikuwa na 102.
Lugola atoa siku tatu raia wa Msumbiji warejeshwe kwao
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment