Naibu waziri wa elimu afurahishwa na matokeo ya Shule iliyoshika nafasi ya 60 kitaifa wilayani Ngorongoro
Naibu waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Mh William
Olenasha ametembelea walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Embarway iliyoko wilayani Ngorongoro mkoani Arusha na
kuwapongeza kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita ambapo shule
hiyo kitaifa ilishika nafasi ya 60 na kimkoa ilishika nafasi ya tatu jambo
ambalo halijawahi kutokea katika Historia ya Wilaya hiyo
Alipofika shuleni hapo Mh Olenasha
alipokelewa na walimu pamoja na kamati ya shule na kukagua madarasa mapya
yanayojengwa na kukagua eneo litakalojengwa Hostel na baadae kuzungumza na
walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya Embarway.
Mh Olenasha amesema ni jambo la
kupongezwa walimu wa shule hiyo ambapo wameandikia historia wilaya ya ngorogoro
pamoja taifa na kuwahimiza kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mitihani
mingine ikiwemo ya kidato cha nne.
“Matokeo ambayo mmepata kuhusiana na
wanafunzi wazazi na wadau wengine ni matokeo ya kihistoria na ni hakika hata
kama imetokea mara moja badi nyie mtaingia kwenye historia kwamba ni kati ya
walimu ambao mmeleta mafanikio makubwa ya elimu wilaya ya ngoronngoro mkoa wa
Arusha na taifa kwa ujumla”Amesema Mh Olenasha
Amesema kuwa hiyo inatokana na
walimu hao kujituma ambao pia wamefuta kumbukumbu ya baadhi ya watu wanaoamini
kuwa shule za serikali hazifanyi vizuri.
Awali akizungumza na wanafunzi wa
Shule hiyo amewataka kusoma kwa bidii zaidi ili waendelee kufanya vizuri katika
matokeo mengine yanayokuja ambapo wanafunzi wamemuahidi Mh Olenasha kuwa
watafanya vizuri zaidi kuliko matokeo hayo ya kidato cha sita.
Naibu waziri wa elimu afurahishwa na matokeo ya Shule iliyoshika nafasi ya 60 kitaifa wilayani Ngorongoro
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment