Kesi ya kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali,
inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman
Mbowe, imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Kesi hiyo imeshindwa kuendelea leo Julai 18, kwa sababu
upande wa mashtaka wanasubiri uamuzi wa maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu,
na washtakiwa hao
Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai jana mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya
kutajwa ili kusubiri maamuzi ya maombi yaliyopelekwa Mahakama Kuu
Nchimbi akisaidiana na Wakili Zainabu Mango na Saimon
Wankyo, alidai kuwa maombi ya awali yaliyowasilishwa Mahakama Kuu,
yalisikilizwa wiki iliyopita na kupangiwa Julai 20, kwa ajili ya kutolewa
maamuzi hivyo wanaomba ipangwe tarehe ya karibu kwa ajili ya kusubiri maamuzi
yatakayotolewa
Hata hivyo, wakati kesi hiyo inatajwa jana, Mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche, hakuwepo mahakamani hapo kutokana na kuuguliwa na
mke wake ambaye amelazwa katika Hospitali ya Bugando
Kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa tunasubiri uamuzi wa
maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu, na washtakiwa hawa," alidai
Nchimbi
Nchimbi baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi Peter
Kibatala akisaidia na Jeremiah Mtobesya, alidai kuwa mapingamizi ya awali
yameshatolewa, hivyo wanaomba mahakama iendelee kuitaja kesi hiyo
"Ni kweli John Heche hayupo mahakamani hapa na nimepata
taarifa kutoka kwa mdhamini wake, kuwa anauguliwa na mke
wake, lakini mdhamini wake anazo fomu za matibabu, ataziwasilisha hapa
mahakamani," alisema Kibatala
Kibatala alifafanua kuwa kama mapingamizi hayo yatafanikiwa
basi kesi itapangwa kwa ajili ya kusikiliza na kama hayatafanikiwa itaendelea kupangwa
kwa ajili ya kutajwa.
Baada ya mdhamini
huyo kuwasilisha fomu hizo mahakamani hapo, upande wa mashtaka walidai kuwa
hawana pingamizi juu ya uthibitisho huo wa matibabu
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Mashauri
aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 25, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa
Viogozi hao wa Chadema, wakiongozwa na mwenyekiti wa chama
hicho, Freeman Mbowe walifungua maombi ya mapitio Mahakama Kuu dhidi
ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), wakipinga uamuzi na amri mbalimbali
zilizotolewa na Mahakama ya Kisutu katika kesi hiyo
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo
ni Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji; naibu makatibu wakuu John Mnyika
(Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).
Wengine ni mbunge wa
Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko;
mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na mbunge wa
Bunda, Ester Bulaya
Katika kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018,
washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo Februari 16, 2018 katika
barabara ya Kawawa, Mkwajuni Kinondoni ambalo wanadaiwa kusababisha
vurugu zilizosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
(NIT), Akwilina Akwiline
Kesi ya Mbowe yakwama tena
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment