Waziri Wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola Ametoa
agizo zito kwa Mkuu Wa Polisi Nchini,IGP Simoni Siro kuhakikisha anampatia
Takwimu za miaka mitano iliyopita kuhusiana na matatizo ya kuuawa kwa madereva
Bodaboda Nchini.
Kauli hiyo ameitoa Julai 23 jijini Arusha alipotembelea kituo kipya cha Polisi kilichopo ,Muriet na kupata fursa ya kuongea na wananchi wakiwemo madereva Wa pikipiki maarufu kwa jina la dereva Toyo
"Namuagiza IGP Siro aliletee orodha ya miaka mitano iliyopita mpaka sasa takwimu za kiwilaya na kimkoa juu ya matukio ya vifo vya madereva bodaboda ili Mimi kama waziri Wa mambo ya ndani niweze kuona matatizo haya yapo eneo gani ili tuweze kujipanga kuhakikisha yanamalizika" Amesema Lugola
Awali baadhi ya madereva Wa Toyo walimweleza jinsi waziri huyo wanavyopata matatizo nyakati za usiku kwa kuuawa na wahalifu Wa matukio hayo.
Wamesema ni vema jeshi la Polisi likawashirikisha pindi wanapofanikiwa kuwakamata wahalifu na kuwapeleka mahakamani ili watambue hatua zaidi zinazochukuliwa kwa wahalifu Wa matukio ya wizi wa pikipiki.
"Zile kesi zinapopelekwa Polisi hatuonyeshwi kila siku sisi tunauawa ila hawa waizi hawaishi sasa sijui wapo sawa kwa sawa na idadi ya Polisi ama vipi????Amesema mwenyekiti Wa madereva Toyo Muriet Akili Mbaga

IGP Sirro atwishwa zigo Jingine na Waziri Lugola Kuhusu Bodaboda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment