Halmashauri ya Meru yawaondoa wafanyabiashara wanaouza mazao katika Maeneo Hatarishi


Halmashauri ya Wilaya ya Meru imeanza zoezi la kuwaondoa Wafanyabiashara wa mazao wanaofanya shughuli zao kwenye maeneo yasiyo rasmi nje ya soko la Tengeru lililojengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao hivyo kusababisha msongamano barabarani na kuhatarisha maisha yao.
Afisa Biashara Halmashauri ya Wilaya ya Meru  ambaye ni Msimamizi wa Masoko Elibariki Abraham  katika wilaya hiyo amesema kuwa zoezi hilo limeanza rasmi baada ya baadhi ya wafanyabiashara kukaidi kutumia soko lililojengwa kwa gharama kubwa na halmashauri huku wao wakiendelea  kupanga bidhaa zao barabarani kinyume cha sheria na taratibu.

Wafanyabiashara wa soko hilo Rose Athumani na Elisifa Boniface  wameunga mkono adhma ya halmashuri kuwaondoa wafanyabiashara barabarani na kuwaingiza katika eneo la soko huku wakisema kuwa jambo hilo limekua likisababisha watu kutofika ndani ya masoko hayo kwani mahitaji waliyapata kwa wafanyabiashara wanaopanga bidhaa barabarani .

 “Kipindi cha mvua wateja wengi hawaingii sokoni wananunua vitu kwa wafanyabiashara walioko barabarani hivyo atupati wateja ni bora serikali iweke utaratibu wote wakae ndani ya soko” Alisema Rose

Baadhi ya Wafanyabiashara waliondolewa barabarani Josephine Izack wamelalamikia kitendo hicho cha halmashauri na kuiomba serikali iwaruhusu ili waweze kujitafutia kipato cha kila siku na kuondokana na ugumu wa maisha.
Halmashauri ya Meru yawaondoa wafanyabiashara wanaouza mazao katika Maeneo Hatarishi Halmashauri ya Meru yawaondoa wafanyabiashara wanaouza mazao katika Maeneo Hatarishi Reviewed by KUSAGANEWS on July 25, 2018 Rating: 5

No comments: