Wakati Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akisema polisi
waliotuhumiwa kuhusika na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT)
Akwilina Akwilini wameachiwa huru, familia ya marehemu imeeleza kuwa itatoa
tamko baada ya kukaa kikao na kuamua
Akwilina
alipigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati viongozi na wanachama wa
Chadema wakiandamana kwenda Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni,
Februari 16 mwaka huu
Kaka wa
marehemu, Richard Akwilini alisema familia yao itakaa kikao kujadili hatua ya
Serikali kuwaachia huru waliotuhumiwa kuhusika na kifo cha ndugu yao
“Ratiba
ikienda sawa kama tulivyopanga, tutapata jibu la uhakika baadaye,” alisema
Richard
Wakati familia
ikisema hayo, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) wameilalamikia kauli ya
Mambosasa ya kuihusisha Chadema na mauaji ya Akwilina.
Baraza hilo lilisema kauli hiyo inalenga
kukiwekea chama hicho vikwazo kwenye uchaguzi mdogo wa Agosti 12
Famili ya Akwilina yakaa kikao, Bavicha walalamika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment