Wanasiasa
wametakiwa kuacha kutetea wananchi wanaovamia maeneo yaliiyotengwa ikiwamo
vyanzo vya maji kwa kuwa wanaharibu mazingira
Hayo
yameelezwa leo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, kwenye kilele cha maadhimisho
ya Siku ya Mazingira na maonyesho ya ubunifu, leo Juni 5, yaliyofanyika katika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini hapa
“Tunapaswa
kukuza uelewa na utashi wa kisiasa kwa uhifadhi wa mazingira kuna maeneo
wananchi wanavamia kwa makusudi, wanatokea wabunge na madiwani
wanawatetea,"amesema
Mama Samia
amesema kila mmoja anapaswa kutafakari namna bora ya kukabiliana na changamoto
katika utunza mazingira ili maisha yaendelee
"Mapambano
ya uharibifu wa mazingira siyo jukumu la Serikali pekee, bali kila mmoja
ashiriki,"amesema
Waziri wa
Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mama Samia,amesema amedhamiria kuwatumia vyema viongozi wa
dini katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
“Wenzetu hawa
wana watu, hivyo watatusaidia kuhubiliri uhifadhi wa
mazingira,"amesema Waziri Makamba
Amesema kuna
matumizi mkubwa ya nishati ya mkaa ambapo wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam
wanatumia kwa asilimia 70 wakati tafiti zikionyesha mkoa huo upo hatarini
kuwa jangwa.
Wanasiasa watakiwa kuacha kutetea wanaoharibu mazingira
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment