![]() |
| NB- Siyo picha halisi ya mtoto katika habari |
Dunia ina mambo ndivyo unaweza
kusema!! Katika hali isiyokuwa ya kawaida
mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Nyarigongo kata ya Mwakitolyo halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga 'Shinyanga Vijijini' mkoani Shinyanga amejifungua
mtoto wa kiume ambaye amekuwa akizungumza wakati akiwa tumboni mwa mama yake.
Mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha
kwa jina la Maria Mpago ameiambia malunde1 blog kuwa licha ya mtoto kuwa na
tabia ya kuzungumza tumboni hata wakati wa ujauzito vipimo vya kitabibu
vilishindwa kubaini kama ni mjamzito licha ya kumsikia mtoto akichezacheza
tumboni.
“Nilipimwa kama nina ujauzito katika
zahanati ya Mwakitolyo lakini mimba haikuonekana... nikaambiwa labda nikajaribu
Kahama lakini nako haikuonekana.... basi nikaendelea kulea mimba..
....Wiki mbili zilizopita siku ya Ijumaa majira ya saa saba usiku nikasikia mtoto akiniongelesha tumboni akisema 'nipeleke msikitini nikaombewe dua,ukinipeleka sasa mimba itaonekana,usiponipeleka itaharibika kwa kuwa mimi ni muislam ndipo kesho yake nikaenda msikitini nikakutana na shehe nikamwelezea kilichotokea akaniombea…na juzi siku ya Ijumaa Juni 1,2018 ndipo nikajifungua nyumbani”,anasimulia Maria,

Licha ya mfululizo wa visa vya mtoto
huyo ,Maria na mumewe wanasema hawana wasiwasi wowote na kwamba hali hiyo ni
hali ya kawaida tu wakidai huenda ni matukio tu yanawatokea hata watu wengine.
Mtoto huyo ambaye amewashangaza
wengi anaendelea kupatiwa huduma mbalimbali za kiafya ikiwa ni pamoja na chanjo
za magonjwa mbalimbali katika zahanati ya Mwakitolyo.
Muuguzi wa zahanati hiyo Tizila
Kijanda anasema hata wao wanashangazwa na visa vya mtoto huyo na kwamba
wanaendelea kumpatia matibabu kama kawaida.
Wakazi wa eneo hilo wamelihusisha
tukio hilo na imani za kidini wakidai hiyo ni mipango tu mwenyezi Mungu kwani
yeye ndiye muweza wa mambo yote.
Malaki Philipo – Malunde1 blog
Maajabu : MAMA AJIFUNGUA MTOTO ANAYEONGEA KAMA MTU MZIMA SHINYANGA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment