Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameshindwa kujizuia na kuhoji muonekano wa
suti za Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kwa kutaka kufahamu kwa nini
pamoja na kuvaa suti nzuri lakini bado zinaonekana na namba ambazo hazieleweki.
Spika Ndugai amehoji hayo wakati
Mbunge huyo akitoa mchango wake katika bajeti ya wizara ya fedha na mipango kwa
mwaka wa fedha 2018/2019.
Wakati akihoji swali lake kwa Mbunge
huyo, Ndugai aliuliza, "Kabla sijakuongezea dakika moja waheshimiwa
wengi wameniandikia kwamba umevaa suti nzuri sana lakini umeweka lebo za ajabu
hiyo 219 ni kitu gani?
Akijibu swali hilo Sugu amesema
"Hii ni namba yangu ya mfungwa jela, ambayo nitaendelea kuvaa kadiri
ambavyo nitajisikia. Kuhusu Suti Mh. Spika wewe unanijua ni kawaida yangu
kupiga suti kali".
Hata hivyo baada ya jibu hilo Spika
Ndugai amemuahidi Mbunge huyo kufuatilia zaidi katika kanuni zake kama
inaruhusiwa kuvaa namba za magereza ndani ya jengo la Bunge.
Hivi karibuni Mbunge huyo kutoka
Mbeya mjini amekuwa akionekana akivaa nguo zenye namba 219 mbele ambapo huwa
akifafanua kwamba ilikuwa namba yake siku alipoingia magereza ya Ruanda baada
ya kuhukumiwa kifungo cha miezi 5 kwa kosa la kutoa lugha chafu dhidi ya Rais
Magufuli
Ndugai aihoji suti ya Sugu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment