Walimu pamoja na wafanyakazi
wakiume katika shule ya Sekondari ya wasichana Moi jijini Nairobi
wametakiwa kufanyikwa uchunguzi wa vinasaba ‘DNA’ ili kubaini watuhumiwa
wa tukio la ubakaji lililofanyika shuleni hapo.
Polisi
wamewaagiza walimu hao wa kiume, pamoja na wafanyakazi wanaoishi ndani
ya shule hiyo kutekeleza zoezi hilo litakalosaidia kurahisha uchunguzi
wa nani mtuhumiwa kwani taarifa zinasema hakuna mgeni aliyeingia usiku
ule zaidi ya watu wa shuleni hapo.
“Uchunguzi huo wa ‘DNA’ utarahisisha kubaini watuhumiwa waliotenda tukio hilo la unyanyasaji wa kijinsia kwa mabinti hao kwani vipimo vya awali vya mabinti vimehifadhiwa”, imesema taarifa ya Polisi.
Gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa tayari maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha uhalifu na mkemia wa serikali hapo jana Jumatatu walichukua sampuli za wafanyakazi wanane wa shule hiyo miongoni mwao walimu 6 ili kufanyiwa ukaguzi wa maabara

Walimu wa kiume kufanyiwa ‘DNA’
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment