Mwendesha mashtaka wa jamhuri,Sabina Silayo aliieleza jana mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo haujakamilika na kuomba ihairishwe hadi tarehe nyingine.
Mara baada ya ombi hilo ndipo hakimu wa mahakama hiyo,Patricia Kisinda alihairisha hadi Juni 18 na kuamuru washtakiwa warejeshwe rumande.
Nje ya Mahakama
Mama mzazi wa Lucas,..amelalamikia jaribio LA kutaka kurubuniwa kwa fedha kwa mtoto wake ili aachane na jambo hilo, hali aliosema hakubaliani nayo ukilinganisha na udhalilishaji aliofanyiwa mwanaye
Watuhumiwa hao walifikishwa hivi karibuni katika mahakama ya wilaya ya Arumeru wakishtakiwa kwa makosa mawili ikiwemo kumvua nguo na kisha kumchukua picha akiwa uchi mwandishi wa habari wa kujitegemea mkoani Arusha,Lucas Myovela.
Washtakiwa hao wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ambapo shtaka la kwanza ni kunyang”anya kwa kutumia silaha kinyume na kifungu cha 287A cha sheria ya kanuni ya adhabu kifungu kidogo cha 16 kilichorekebishwa mwaka 2002.
Mnamo Mei 13 mwaka huu katika maeneo ya Sakina jijini Arusha washtakiwa hao kwa pamoja walimwimbia Myovela simu aina ya Tecno C7 yenye thamani ya sh,300,000,simu aina ya Samsung yenye thamani ya sh,50,000 pamoja na fedha taslimu kiasi cha sh,75,000.
katika kosa hilo washtakiwa hao kwa pamoja walihamisha kiasi cha sh 9,500 kwa njia ya Mpesa kutoka kwenye nambari 0754-677472 mali ya Mvyovela na kabla ya kufanya tukio hilo walitumia silaha aina ya panga na mkanda wa plastiki kwa lengo la kumtishia na kisha kubaki na mali hizo.
Katika kosa la pili washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kufanya matendo ya kikatili na udhalilishaji kinyume na kifungu cha sheria cha 138 A cha sheria ya kanuni ya adhabu kifungu kidogo cha 16 kilichorekebishwa mwaka 2002.
Katika kosa hilo washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa mnamo Mei 13 mwaka huu katika maeneo ya Sakina jijini Arusha wanadaiwa kufanya matendo ya kikatili ya udhalilishaji ambapo walimvua nguo Myovela na kisha kumchukua picha akiwa uchi.
No comments:
Post a Comment