|
Nairobi, Kenya. Rais Uhuru
Kenyatta Jumatatu aliwasimamisha wakuu wote wa Idara za Manunuzi ya Umma na
Vitengo vya Uhasibu katika wizara zote wakisubiri kufanyiwa upya uhakiki,
hatua inayolenga kung’oa ufisadi kwa watumishi wa umma serikalini
Hatua hii imekuja siku chache
tangu Rais Kenyatta atoe tangazo wiki iliyopita kwamba wote wanaoshikilia
ofisi za umma wajiandae kufanyiwa uhakiki ili kujua uaminifu wao. Kenyatta
aliwaonya wakuu hao kwamba wale wote watakaoshindwa kufikia vigezo vilivyowekwa
vya uhakiki watasimamishwa na baadaye kushtakiwa ikiwa watapatikana wana
makosa ya ukiukwaji wa sheria za manunuzi ya umma
Pia, hatua hii imekuja katika
kipindi ambacho watu kadhaa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na kashfa zilizoandikwa
sana kwenye vyombo vya habari na kuwaudhi wananchi hali iliyomlazimu rais
kuchukua hatua hiyo
Watu 54 washtakiwa
Watu 54, wakiwemo katibu mkuu wa
utumishi wa umma, walikamatwa na kushtakiwa wiki iliyopita wakidaiwa kuhusika
katika wizi kutoka Shirika la Taifa la Huduma kwa Vijama (NYS
Shirika hilo lililoko chini ya
Wizara ya Vijana ambalo lilianzishwa kwa lengo la kukabiliana na ukosefu wa
ajira, linahusika katika kufundisha vijana kufanya kazi katika miradi tofauti
kuanzia ujenzi hadi kudhibiti watu barabarani
Lakini kwa bahati mbaya, hazina ya
NYS iliingiliwa na wahuni. Mwaka 2015, aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi Anne
Waiguru alijiuzulu baada shinikizo kutoka kwa wananchi kutokana na wizara
yake kudaiwa kukubuhu katika rushwa, na yeye binafsi alihusishwa na wizi wa
Sh791 milioni (dola 8 milioni) kutoka NYS. Lakini mwaka 2017 Waiguru
alichaguliwa kuwa gavana wa Kaunti ya Kirinyaga katika mkoa wa kati
|
Wakuu wa manunuzi, uhasibu wasimamishwa Kenya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment