eshi laokoa wanawake watumwa wa ngono


Nigeria. Jeshi Jumatatu lilisema kuwa liliwaokoa wanawake 58 waliokuwa wakitumika kama watumwa wa ngono na Boko Haram huko Modu Kimeri, eneo la Serikali ya mitaa katika Jimbo la Borno

Naibu Mkurugenzi wa Uhusiano na Uendeshaji wa Kamandi ya Operesheni Lafiya Dole, Onyema Nwachukwu alisema mjini hapa kwamba mbali ya wanawake hao, pia jeshi liliwaokoa watoto 75 na wanaume 15

Nwachukwu alisema wanawake hao waliokolewa na askari wa Brigedi ya 21 wakishirikiana na Kikosi Kazi Maalumu cha Raia kilichoandaliwa katika operesheni hiyo iliyopewa jina la Operesheni Lafiya Dole

"Jeshi liliwaokoa mateka hao katika Operesheni Safishasafisha Jumapili ya Juni 3, 2018, ili kulisafisha kwa ujumla eneo lote la Bama, Modu Kimeri na Gulumba Gana walikokuwa wakikaa magaidi wa Boko Haram waliokuwa wakikimbia kutoroka vita vikali katika Visiwa vya Ziwa Chad na mipaka ya kaskazini ya Jimbo la Borno

"Mateka waliokolewa, wamo wanaume 15, wanawake 58 na watoto 75 waliogundulika wakati wakichujwa na kuhojiwa na askari wa Operesheni Lafiya Dole na mashirika mengine ya usalama, kwamba magaidi ya Boko Haram waliwadhalilisha kingono wanawake na waliwatumia kama watumwa wa ngono," alisema

eshi laokoa wanawake watumwa wa ngono eshi laokoa wanawake watumwa wa ngono Reviewed by KUSAGANEWS on June 05, 2018 Rating: 5

No comments: