Makonda atatumia askari 400 wa JKT operesheni usafi wa mazingira Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ataanzisha operesheni ya usafi wa mazingira itakayoshirikisha askari wa Jeshi la Kujenga Taifa 400 ili kuhakikisha jiji hilo  linakuwa safi tofauti na lilivyo sasa

“Naomba unifikishie salamu hizi kwa Rais John Magufuli tutawakamata, hapa ni askari wa JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) 400. Ziba masikio nataka niendeshe operesheni ili jiji linyooke na liwe safi," amesema Makonda

Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 5 2018 wakati wa maadhimisho ya siku mazingira duniani ambayo kitaifa yamefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Makonda amemweleza Samia kuwa bado  usafi katika jiji la Dar es Salaam ni tatizo na kwamba watu ni wachafu na wanatia aibu

"Hapa unawaona ni nadhifu, lakini huko walikotoka hawajaacha mazingira vizuri. Makamu wa Rais naomba uzibe masikio kidogo kwa hii operesheni." 
Makonda atatumia askari 400 wa JKT operesheni usafi wa mazingira Dar Makonda atatumia askari 400 wa JKT operesheni usafi wa mazingira Dar Reviewed by KUSAGANEWS on June 05, 2018 Rating: 5

No comments: