Serikali
imesema inaandaa utaratibu maalumu wa kutoa ajira za moja kwa moja kwa
wanafunzi wa fani mbalimbali za ufundi kutoka vyuoni ili kuepusha usumbufu
wanaopata katika kutafuta ajira mara baada ya kuhitimu masomo yao.
Hayo yamesemwa leo Juni 1, 2018 Bungeni, Jijii Dodoma na
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na Walemavu,
Anthony Mavunde na kuongeza kuwa serikali itawaunganisha moja kwa moja wahitimu
hao pamoja na wadau mbalimbali nchini ambao hutoa nafasi za ajira katika fani
za ufundi.
“Tunachokifanya
kama Serikali kwanza kabisa kwa kushirikiana na Sekta binafsi ambapo pindi
nafasi zinapopatikana huwa tunaunganisha moja kwa moja na vyuo vyetu vya ufundi
ili vijana hawa waweze kupata nafasi za ajira za moja kwa moja, sisi kama
Serikali tutaona namna ya kuunganisha vyuo vyetu vya ufundi pamoja na waajiri
nao wapate nafasi za moja kwa moja” amesema Mavunde
Mavunde
ameongeza kuwa serikali itatumia mfano wa baadhi wa vyuo vya ufundi kikiwemo
chuo cha Don Bosco ambacho hufanya kongamano wadau wa fani za ufundi ili kuweza
kutoa fursa za ajira kwa vijana wanohitimu katika chuo hicho.
Kwa upande
mwingine Naibu Waziri huyo amedai kuwa Serikali imeweka vituo vya kulea vijana
ambavyo ni Sasanda (Mbeya), Ilonga (Morogoro) na Kilimanjaro lengo likiwa ni
kuandaa vijana kuwa na sifa za kuajirika na pia Serikali imetenga mfuko wa
maendeleo ya vijana ili kutoa mikopo kwa vijana.
Wahitimu sasa kuajiriwa moja kwa moja - Mavunde
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment