Wahanga
watatu wa tiba iliyodaiwa kutibu Virusi vya UKIMWI ya aliyekuwa Rais wa
Gambia, Yahya Jammeh wamemshitaki Rais huyo aliye uhamishoni kwa kudai kuwa
haki zao za kibinadamu zilivunjwa.
Kwa mujibu wa mtandao wa African News, umesema kuwa
Wahanga hao waliojulikana kama Ousman Sowe, Lamin Ceesay, na Fatou Jatta madawa
hayo yalisababisha hali zao kuwa mbaya na wengine kupoteza maisha.
Aidha wahanga hao wameweka bayana kwamba awali walikuwa na uoga wa kumshitaki
akiwa Rais lakini sasa ukweli lazima ujulikane.
Wahanga hao
wamedai kuwa tiba hiyo iliwaathiri sana kisaikolojia kwani wakati mwingine
aliwapaka dawa za mafuta katika vipindi vilivyooneshwa kwenye televisheni.
Rais Yahya
Jammeh alianzisha tiba hiyo ya asili mwaka 2007 akidai inatibu UKIMWI. Tiba
ambayo iliwataka wagonjwa hao kuacha kunywa dawa za kupunguza makali ya VVU za
ARV na kunywa madawa ya asili yaliyowasababishia kutapika.
Hata hivyo
imeelezwa kuwa Programu hiyo mbadala ilirudisha nyuma harakati za kupambana na
ugonjwa wa UKIMWI katika nchi hiyo ambayo iko nyuma katika viwango vya tiba kwa
mujibu wa UNAIDS.
Waathirika wa Ukimwi wamshtaki Rais Mstaafu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment