Mbunge ataka serikali itumie kipimo cha mate

Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdallah Salim ameibuka na kuibana serikali kuwa ni lini itaanza kutumia teknolojia ya kisasa ya mate katika kutambua waathirika wa Virusi Vya UKIMWI kama wanavyofanya nchi nyingine duniani na kuachana na ile ya kutoa damu. 
Mbunge Masoud ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma Mei 31, 2018 wakati alipokuwa anauliza swali la nyongeza kuwa hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI katika Jiji la Dodoma yanaongezeka kwa kasi ambalo alikuwa amelielekeza kwenye Wizara ya Afya.

Akijibu swali hilo, Waziri Ummy Mwalimu amekiri kuwepo kwa ongezeko la  maambukizi ya VVU ambapo yamepanda kuanzia mwaka 2012 hadi 2017 na katika mkoa wa Dodoma maambukizi yameongezeka kutoka asilimia 2.4 hadi tano sawa na mikoa ya Tanga na Mwanza na wanafanya utafiti maalum ili kubaini sababu za

"Ni kweli tumekuwa na changamoto ya watu kuwapata kupima hasa wanaume na tumeona njia ambayo itaweza kusaidia wanaume kupima Ukimwi ni njia ya mtu kujipima mwenyewe. Kwa sasa sheria iliyopo imekuwa kikwazo kutimiza hilo, hivyo wataandika barua kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ili kuwasilisha muswada wa mabadiliko ya sheria ambayo pamoja na mambo mengine, itaruhusu mtu kujipima VVU ikiwamo kwa njia ya mate ili ndani ya dakika 15 apate majibu", amesema Ummy.

Pamoja na hayo, Ummy Mwalimu ameendelea kwa kusema "tunaamini mtu akijipima na kujua majibu itakuwa kichocheo cha kwenda katika kituo cha afya ili kuthibitika na kuingizwa kwenye mpango wa dawa. Nasisitiza dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI (ARV) zipo kwa asilimia 100, watu wapime Ukimwi tena si kifo".

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amesema serikali imeridhia mkakati wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wa kupima VVU na kutibu bila kuzingatia kiwango cha kinda mwilini (CD4).
 

a

Mbunge ataka serikali itumie kipimo cha mate Mbunge ataka serikali itumie kipimo cha mate Reviewed by KUSAGANEWS on June 01, 2018 Rating: 5

No comments: