Mwanafunzi
mmoja nchini Kenya ameunda gari linalotumia kawi ya jua, gari ambalo limekuwa
likiwavutia watu kutokana na kubadili jua kuwa umeme.
Samuel Karumbo, 30, ni mwanafunzi katika chuo cha
mafunzo anuwai cha serikali mjini Kitale, Magharibi mwa Kenya, amesema gari
lake, ambalo lina mitambo mitatu ya sola iliyobandikwa, linaweza kusafiri
umbali wa kilomita 50 kwa siku.
Karumbo
anasema mchana, sola huchukua nishati ya jua na kuibadilisha kuwa umeme ambao
unahifadhiwa kwenye betri ambazo ndizo zinazotumiwa moja kwa moja kuliendesha
gari hilo na pia wakati jua halijawaka sana.
Gari hilo
lina uzani wa kilo 120 na kwenye mteremko hutumia mvuto wa nguvu za ardhi
badala ya umeme. Nguvu hutumia tu kwenye kupanda milima au maeneo yenye
miinuko.
Gari inayobadili Jua kuwa umeme
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment