Wabunge wa CCM wamempongeza Rais
John Magufuli anavyoshughulikia sekta ya madini ikiwamo kuzuia usafirishaji wa
mchanga wa madini ya dhahabu ‘makinikia’ nje ya nchi.
Wabunge hao Goodluck Mlinga (Ulanga)
na Sixtus Mapunda (Mbinga Mjini) wamesema hayo leo Juni 1, 2018 bungeni wakati
wakichangia bajeti ya madini ya mwaka 2018/19.
“Nampongeza Rais (Magufuli) kwa
kuzuia makinikia kupeleka nje ya nchi, Tanzania ni nchi ya nne kwa uzalishaji
wa dhahabu kwa nchi za Afrika na duniani. Katika nchi matajiri wa uzalishaji wa
mali tupo lakini mafanikio ya wananchi na Serikali tuko chini,” amesema Mlinga.
Amesema anampongeza Rais kwa kujenga
ukuta katika mgodi wa Mirerani kwani ni madini adhimu.
“Tanzania ni nchi ya nne kwa
uzalishaji wa gesi katika bara la Afrika. Lakini katika nchi masikini tupo,”
amesema.
Akiendelea kuchangia, Mlinga
amesema, Rais anapaswa kufanya mabadiliko katika wizara ya madini kwani
watendaji wake wamesababisha haya.
Naye Mapunda amesema alichokifanya
Rais ni jambo kubwa kwani tuna madini mengi lakini yalikuwa hayatunufaishi.
“Tuko katika mpito kutengeneza mfumo
bora wa kutunufaisha na yote yanahitaji ushirikiano na kupeana moyo. Biashara
ya dhababu ni ya familia kubwa na jinsi ya kuiingia inahitaji kutumia ubongo
mkubwa sana,” amesema Mapunda na kuongeza:
“Ili kuingia kupambana nao inahitaji
kuwa na mfumo mzuri na Serikali inapoanza kutengeneza sheria, hawa hawawezi
kukubali, lazima watatuhujumu.”
Wabunge CCM Wammwagia Sifa Rais Magufuli Bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment