Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Mkurugenzi
Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, MaxenceMelo na Mwanahisa wa
mtandao huo, Micke William baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa aliwaachia huru
washtakiwa hao leo Juni 1, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi
sita wa upande wa mashtaka na kuona ushahidi huo hauna mashiko
“Hakukuwa na ushahidi unaoeleza moja kwa moja wa barua hiyo
ya kuwataka watoe taarifa za kampuni yao na ushahidi huo una mashaka?” amesema
Mwambapa
Katika kesi hiyo Melo na mwenzake wanadaiwa kuzuia
uchunguzi wa jeshi la polisi kwa kukataa kutoa taarifa za kampuni yao
Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi
Mutalemwa,amedai kuwa baada ya usajili, kampuni hupewa taarifa za siri ambazo
huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika hivyo washtakiwa hao walikuwa
na uwezo kuona taarifa kwenye mfumo wao
Kishenyi amedai kuwa kufuatia jitihada hizo za Mkuu wa
Upelelezi Kanda Maalum(ZCO) za kuwataka washtakiwa kutoa taarifa muhimu na wao
kukataa walikamatwa na kufikishwa mahakamani
Mahakama yamuachia huru mmiliki Jamii Forum
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment