KERO YA MAJI TANZANIA KUWA HISTORIA


Naibu Waziri wa maji Mhe.Jumaa Awesso amesema Serikali inaendelea vyema na jitihada zake za kuhakikisha Watanzania wote wanapata maji safi na salama ya kunywa.

Naibu Waziri Awesso amesema kuwa hilo linawezekana hasa baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha  zaidi ya shilingi Bilioni mia saba kwa wizara hiyo

Amesema kinachotakiwa sasa ni miradi ya maji ambayo ipo katika utekelezaji wake isimamiwe vyema na wahusika ili iweze kutimiza malengo yake

Naibu Waziri Awesso alikuwa akijibu maswali Bungeni ambayo yalikuwa yameelekezwa kwa wizara ya maji.
KERO YA MAJI TANZANIA KUWA HISTORIA KERO YA MAJI TANZANIA KUWA HISTORIA Reviewed by KUSAGANEWS on June 01, 2018 Rating: 5

No comments: