Mbunge wa Mbeya Mjini, (Chadema) Joseph Mbilinyi (Sugu)
ameitaka Serikali kuwasaidia askari magereza wanaostaafu kulipwa mafao bila ya
usumbufu kwani wanapostafu husubiri hadi zaidi ya miaka miwili
Akizungumza leo Juni 4 bungeni, Sugu amesema Serikali
huwasumbua askari hao bila sababu za msingi wakati wanafanya kazi ngumu ya
kuwatunza wahalifu
“Mheshimiwa spika, serikali inasema kuhusu askari hawa ambao
wamekuwa wakisumbuliwa kutolipwa stahiki zao baada ya kustaafu wakati polisi
wanaotukamata na kutupiga wanalipwa mapema lakini wahalifu wote wanarundikwa
magereza kwa hiyo hawa wanakuwa na kazi ngumu,” amesema Sugu
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuwa swali hilo licha ya
kuwa ni refu lakini ameamua kuliacha lijibiwe kwani limeulizwa na mtu mzoefu
kuliko maswali mengine yanayoulizwa kwa ubabaishaji
Akijibu swali hilo na swali la msingi kutoka kwa mbuge wa
Viti Maalum Lucy Mlowe (Chadema), Naibu Waziri wa Fedha Dk Ashatu Kijaji
amesema Serikali inalipa mafao kwa wastaafu wote bila ya upendeleo na kuwa
katika kipindi cha hivi karibuni, zililipwa jumla ya Sh 282 bilioni kwa
wastaafu mbalimbali
Naibu waziri amewaondoa hofu pia watumishi wote walioajiriwa
katika miaka ya 1980 kupitia Serikali Kuu lakini wakati ule hapakuwa na makato
ya mfuko wa kijamii
Sugu ‘ang’ang’ania’ mambo ya magereza
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment