JPM haridhishwi na mwenendo wa Benki ya Kilimo


Rais John Magufuli amesema hajaridhika na utendaji kazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

Akizungumza  leo Juni 4 katika hafla ya uzinduzi wa Awamu ya pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP II) Rais Magufuli amesema hafahamu  kama mkurugenzi wa benki hiyo yupo ofisini na anafanya kazi

Amesema Serikali iliipa mtaji wa Sh60bilioni  TADB, mwaka 2017  baada ya kukopa zaidi ya Sh207.05 bilioni kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya kuiongezea mtaji benki hiyo

Amesema  tayari benki hiyo imeshatoa awamu ya kwanza ya mkopo huo ambayo ni Sh102.7 bilioni lakini  bado utoaji wa mikopo kwa wakulima umekuwa ni wa kusuasua badala yake wamejikita kufanya biashara na benki nyingine

Magufuli amesema Serikali inakopa wakakopeshwe wakulima lakini benki hiyo inachukua fedha hizo na kwenda kufanya biashara na benki nyingine

Amesema kuanzia Januari hadi Desemba, 2017, benki hiyo ilifanya biashara na benki nyingine kwa kiasi cha Sh 82.3bilioni

“Ina maana wakulima kwa mwaka huo hawajapata mkopo wowote kwenye benki ya Serikali, sifahamu kama mkurugenzi huyo bado yupo anafanya kazi

“Hili ni suala la wizara ya fedha, suala la benki kuu, hamuwezi, wakulima wanahangaika hawakopeshwi fedha zao,” amesema Magufuli.
JPM haridhishwi na mwenendo wa Benki ya Kilimo JPM haridhishwi na mwenendo wa Benki ya Kilimo Reviewed by KUSAGANEWS on June 04, 2018 Rating: 5

No comments: