JPM: Watendaji tuseme kwa uwazi yanayohusu kilimo


Rais John Magufuli amewataka watendaji kutoa taarifa za masuala ya kilimo kabla hawajasemwa

Ametoa maagizo hayo leo Juni 4 alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya programu ya kuendeleza kilimo
Amesema wamekuwa wakifanya juhudi mbalimbali kuboresha sekta ya kilimo ikiwamo kutafuta fedha kwa ajili ya kuiendeleza, lakini kuna wanaosema hazitengwi fedha kwa ajili ya sekta hiyo

“Tunapeleka lakini inawezekana hazitoshi, wengi wanaosema hatupeleki wanaangalia sekta ya kilimo kwa upekee na kusahau baadhi ya fedha za kilimo zipo kwenye wizara ya maji, nishati, mifugo na  uvuvi, Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura) na ardhi, ”amesema

Amesema wanasemwa kwa sababu waliopo serikalini hawasemi mambo kama hayo, badala yake wamekaa kimya na hawatoi taarifa za ukweli katika hayo wanayosemwa

“Tusikae kimya tukaendelea kusemwa, tukifanya hivi yale tunayosemwa yataonekana ya ukweli, niwaombe sana viongozi wenzangu wote hadi wakuu wa mikoa masuala mbalimbali ya kilimo yanapoulizwa tuwe tunatoa majibu na ikiwezekana tuyatoe kabla ya kusemwa,” amesema Dk Magufuli.
JPM: Watendaji tuseme kwa uwazi yanayohusu kilimo JPM: Watendaji tuseme kwa uwazi yanayohusu kilimo Reviewed by KUSAGANEWS on June 04, 2018 Rating: 5

No comments: