Mke wa
marehemu bilionea, Erasto Msuya, Miriam Mrita ameiomba Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kuunda tume kuichunguza kwa kina kesi ya mauaji inayomkabili
akidai kuna uonevu unaoendelea
Miriam
amewasilisha ombi hilo leo Juni 4 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba mara
baada ya wakili wa serikali, Patrick Mwita kuiambia mahakama kuwa kesi
ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, lakini jalada halisi lipo kwa Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP) na kuomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa
Baada ya Mwita
kueleza hayo, Miriam alinyoosha mkono ambapo hakimu Simba alimruhusu kuongea
Miriam
alisimama na kuiambia mahakama kuwa huu ni mwaka wa pili sasa wanaendelea
kusota mahabusu.
"Mimi ni mama mjane, mume wangu ameuawa,
mimi nipo mahabusu gerezani kwa miaka miwili, kama mama sijui watoto wangu
wanaendeĺeaje huko nje." Ameongea Miriam
Ameongeza kuwa
amechoshwa na wimbo wa upande wa mashtaka kuwa upelelezi bado haujakamilika
"Mtu
ukishafiwa na mume kuna vurugu mechi zinaendelea huko nje, naomba iundwe tume
ya uchunguzi wa kina ya kuichunguza kesi hii kwa sababu kuna uonevu ambao
unaendelea."Ameeleza Mrita
Amebainisha
mahakamani hapo kuwa kesi yake ipo kifamilia zaidi na kuomba iangaliwe zaidi na
kwamba watagundua mambo mengi zaidi
Anadaiwa
kumuua kwa makusudi dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Anathe
Msuya Mei 25, 2016 huko Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Bilionea Msuya ataka tume ya uchunguzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment