Dk Faith Kundy aliyekuwa akiwahudumia pacha Maria na
Consolata katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa ameeleza jinsi Consolata
alivyofariki dunia kati ya dakika 10 hadi 15 baada ya mwenzake kufariki.
“Wakati tunampa Maria
huduma ya kwanza na namna alivyokuwa anatapatapa, Consolata alianza kuhisi hali
hiyo ndio maana alikuwa akinisukuma na kusema tuache, tuache, tuache na
nilikuwa nawaambia pumua... pumua... pumua... niliwasisitiza hivyo,” amesema Dk
Kundy
Ameeleza kuwa katika kuungana kwao kuna viungo vilivyokuwa
pamoja
“Anaweza kula Consolata na Maria akasema ameshiba na hata
suala la maumivu ataanza kulalamika Consolata na baada ya muda mfupi Maria
analalamika,” amesema
Daktari huyo ameeleza kuwa tangu walipowapokea pacha hao
kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hawakuwa kwenye hali nzuri kwa sababu
Maria alikuwa akitumia oksijeni kupumua
“Kwa hiyo walikuwa chini ya uangalizi na tulikuwa tunaangalia
hali zao na kama kuna tatizo basi tunawasaidia,” amesema
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa,
Museleta Nyakiroto alipoulizwa kuhusu iwapo mmoja angeendelea kuwa hai kwa muda
mrefu, amesema pacha hao walikuwa na mshipa mmoja mkubwa wa damu uliokuwa
ukiwasaidia wote wawili
Dk Nyakiloto aliwaeleza waandishi wa habari Jumamosi, Juni 2
kuwa pacha hao walifariki dunia wakipatiwa matibabu katika chumba cha uangalizi
maalumu (ICU).
“Tangu wafikishwe hospitalini hatukuwahi kuona wakibadilika
kiafya kiasi kile. Jana (juzi) hali yao ilikuwa tofauti sana. Maria ndiye
alianza kufariki na baada ya dakika 10 alifuata Consolata,” alisema
Daktari aeleza Consolata alivyofariki baada ya mwenzake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment