“Dk Faith sisi
tunakufa,” hiyo ndio ilikuwa kauli ya mwisho ya Consolata Mwakikuti wakati
pacha mwenzake, Maria akiwa katika hali ya umauti
Dk Faith Kundy
ndiye aliyekuwa akiwahudumia pacha hao katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa mpaka
dakika ya mwisho walipofariki dunia juzi usiku.
Akizungumza na
Mwananchi jana Jumapili, Juni 3 daktari huyo alisimulia hali ilivyokuwa katika
dakika za mwisho za uhai wa pacha hao na kueleza kuwa baada ya kuona hali ya
mwenzake imebadilika, Consolata alianza kumsukuma (Dk Faith) akimtaka aache
kuwapatia matibabu, akieleza kuwa alikuwa katika maumivu makali na tayari
alishakata tama
Awali, Dk
Faith alisema juzi saa kumi na moja jioni alipigiwa simu kuwa hali ya pacha hao
imebadilika
“Nilikimbia
hadi wodini kwa ajili ya kuwaona na kuwahudumia. Nilipofika niliwaona wauguzi
na madaktari wengine wakiendelea kutoa huduma ya kwanza hivyo niliungana nao
kwa ajili ya kuokoa uhai wao,” alisema
“Kuna dawa
niliwapatia ambazo huwa zinamsaidia mtu anapokuwa anakosa hewa, Maria alikuwa
ameanza kubadilika kabisa na kwa wakati huo hakuwa na ufahamu. Ilikuwa hata
ukimuita haitiki wala kuonyesha kama anasikia.”
Dk Faith
alisema wakati huo mfumo wa upumuaji wa Maria ulikuwa chini kabisa hivyo baada
ya huduma hiyo, alirejea kwenye hali yake ya kawaida
“Hapo Maria
alifungua macho, ukimuita anaitika na akawa na hali nzuri baada ya huduma,”
alisema
Aliendelea
kusimulia kuwa baada ya hali zao kuwa vizuri aliendelea kuwahudumia wagonjwa
wengine hadi saa moja jioni alipoitwa tena na kuambiwa hali za pacha hao
zimebadilika
“Nilipoenda
kwa mara ya pili, Maria alikuwa kwenye hali mbaya kama ile ya kwanza na safari
hii hakuweza kupona. Ilikuwa kama saa mbili usiku sikumbuki vizuri dakika ila
ndio muda ambao Maria alitutoka,” alisema
Daktari huyo
alisema Maria akiwa kwenye umauti, Consolata pia alianza kutetemeka na
kulalamika maumivu makali mwili mzima
“Alikuwa
anaona kama hamsikii ‘ham-feel’ mwenzake na akawa ananisukuma huku akiniita kwa
jina’ ‘Dk Faith sisi tunakufa’ aliniambia akisisitiza niwaache. Maria hakuweza
kuongea chochote dakika za mwisho na wakati huo Consolata anasema hivyo Maria
alikuwa tayari ameshafariki.”
Consolata alivyomuaga daktari wakati akifariki
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment