Pacha
walioungana Maria na Consolata wanatarajiwa kuzikwa Jumatano katika makaburi ya
viongozi wa dini ya Roman Katoliki, Tosamaganga Mkoani Iringa
Pacha hao
wanaandaliwa jeneza moja lenye mfumo wa watu wawili huku misalaba ikiwa miwili
na kaburi moja.
Akizungumzia ratiba ya maziko ya pacha hao,
leo Juni 4, Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Richard Kasesela alisema wapo
katika hatua za mwisho za maandalizi ya mazishi hayo
Amesema ibada
ya kuaga mapacha hao itafanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Kikatoliki
cha Ruaha (Rucu) kuanzia saa mbili asubuhi kabla ya safari ya Tosamaga
kwa ajili ya mazishi
"Taratibu
zinaendelea na tumekubaliana kutengeneza jeneza moja lenye mfumo wa watu
wawili, tutakuwa na misalaba miwil lakini watazikwa kaburi moja," amesema
Kasesela
amesema kuwa tayari ndugu wa pacha hao kwa pande zote mbili wamewasili na
kwamba saa kumi jioni watakutana tena kupanga bajeti ya msiba.
Jinsi jeneza la Maria na Consolata litakavyokuwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment