Bodi ya Mikopo
ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesitisha mpango wa kutoa mikopo kwa
wanafunzi wanaosoma stashahada (diploma) kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019 kama
ilivyokuwa imetangaza Mei 10 mwaka huu
HESLB ilitoa
mwongozo unaosimamia utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 ambao ulieleza
kuwa ingeanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na kuwa utaratibu wa
kuomba mikopo hiyo ungetolewa baadaye
Hata hivyo,
taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru
inasema hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha kuwa kiasi chote cha Sh427.5
bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2018/2019
kinaelekezwa kwa wanafunzi wenye mikopo hivi sasa na waombaji wapya wahitaji
ambao wana sifa za kujiunga na kozi za shahada tu ambao ndiyo walengwa wakuu
“Hivyo basi,
tunatoa wito kwa wanafunzi wote wenye sifa za kujiunga na masomo ya shahada
katika taasisi za elimu ya juu na ambao ni wahitaji wa mikopo kuhakikisha
wanasoma kwa makini mwongozo wa utoaji mikopo na kuuzingatia,” inasema taarifa
hiyo
Kwa mujibu wa
takwimu za mwaka 2017/2018, takribani maombi 10,027 ya mikopo yaliyowasilishwa
Bodi ya Mikopo yalikuwa na upungufu kama vile kutosainiwa, kutokuwa na
viambatanisho sahihi
Bodi yasitisha mikopo kwa wanafunzi wa diploma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment