Watu watano wanaosadikiwa ni majambazi, wamevamia nyumba ya
mfanyabiashara wa ng’ombe mkoani hapa, Gwaya Ramadhan na kumpora Sh39.8 milioni
Majambazi hayo yakiwa wamefunika sura zao na vitambaa vyeusi
huku wakiwa na silaha zinazodaiwa kuwa SMG, walimvamia mfanyabiashara huyo
nyumbani kwake mtaa wa Mwayunge, kata ya Igunga Mjini wilayani Igunga Juni 2.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa alisema
polisi wanaendelea kuyasaka majambazi hayo na kuwataka wananchi kutoa
ushirikiano watakapopata taarifa yalipo
Akizungumzia tukio hilo, Ramadhan alisema lilitokea Jumamosi
saa 1:00 jioni wakati akifuturu na familia nyumbani kwake
Ramadhan alisema majambazi hayo baada ya kufika nyumbani
yaligawanyika sehemu tatu; moja lilibaki getini, jingine lilimteka mmoja wa
mtoto wake ili alionyeshe sehemu ya kuzimia taa huku jingine likimuamuru atoe
fedha
Alieleza kuwa aliwagomea lakini mmoja wao alitoa amri kwa
aliye na bunduki ampige risasi, hali iliyomlazimu kutii kwa kuwaonyesha fedha
kwenye gari yake alipokuwa amezihifadhi
Majambazi yampora Sh39 milioni mfanyabiashara wa ng’ombe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment