Shekh Mkuu awapongeza kundi la Friends Of Batuli kwa msaada waliotoa kwa Wajane.


Shekh mkuu wa mkoa wa Arusha Shaban Bin Juma amepongeza kikundi cha friends of batuli ambacho kimejitolea misaada mbalimbali ya vyakula kwa ajili ya wanawake wajane 21 wanaosali katika msikiti wa migungani ,pamoja na vitabu vya madrasa kwa ajili ya watoto 78 wanaosoma katika msikiti huo kata ya Sokoni One jijini Arusha.

Akizungumza Shekh Juma Amesema kuwa kundi hilo lilichofanya ni ibada ambayo ndiyo inayompa mtu kuonekana ana roho ya namna gani mbele ya watu kwa kuwa hata vitabu vitakatifu vimefafanua juu ya mtu anayetoa msaada kwa asiyejiweza anapata dhawabu nyingi.

Amesema kuwa kundi hilo limetoa kitu ambacho kiko ndani ya uwezo wao na wanaweza kuona kuwa ni jambo la kawaida lakini wametengeneza mapenzi mema na jamii inayowazuunguka 

“Jambo hili linajenga mapenzi mema katika jamii yetu na maana yake tutakuwa tumeipa ulinzi miji yetu mitaa yetu na nchi yetu, haya kadri yanavyofanyika ni mambo yanayokinga shari sidhani kama yupo mtu binadamu aliye na akili aliyetendewa wema hata kidogo Yule aliyemtendea wema akawa adui yake kupeana hidaya ni jambo linalotekekeza mapenzi katika jamii”Alisema Shekh Juma

Ameongeza kuwa licha ya kuwa kikundi hicho ni watu wa dini mbalimbali lakini hawakutanguliza udini wala ukabila bali wameungana na kufanya utu ambao amesema hakuna Dini bila ubinadamu kwanza.

Kwa upande wa msemaji wa Friends of Batuli Bi Batuli Kisaya amesema kuwa imekuwa ni desturi yao kusaidia watu wasiojiweza wakiwemo watoto wanaoishi mazingira magumu pamoja na wajane ambapo ndiyo lengo kuu la kundi hilo.

Batuli amesema licha ya kuwa na changamoto lakini walichonacho kadri ya uwezo wao wanajitolea ambapo vitu hivyo walivyoto vina dhamani ya shilingi laki saba na nusu 

Nao akina mama wajane waliopata misaada hiyo wamelipongeza kundi hilo ambapo wamesema kuwa maombi yao kwa mwenyezi Mungu ni kula vitu halali ambavyo vinatoka kwenye mikono salama hivyo wanaamini Mungu amesikia maombi yao
Shekh Mkuu awapongeza kundi la Friends Of Batuli kwa msaada waliotoa kwa Wajane. Shekh Mkuu awapongeza kundi la Friends Of Batuli kwa msaada waliotoa kwa Wajane. Reviewed by KUSAGANEWS on June 03, 2018 Rating: 5

No comments: