Mbunge wa
Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kesho Juni 4, 2018 atafanyiwa upasuaji
wa 21 wa kuunga goti la mguu wake wa kulia huku akiwataka Watanzania kumuombea
Upasuaji huo
ni mwendelezo wa upasuaji ambao amekuwa akifanyiwa katika Hospitali ya Nairobi
nchini Kenya alikokuwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa katika
makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, 2017.
Alipatiwa
huduma za awali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Lissu ameeleza
hayo leo Jumapili Juni 3, 2018 kupitia taarifa aliyoitoa katika ukurasa wa
mtandao wa kijamii wa Instagram, akiambatanisha na picha yake akiwa amelala
wodini kando ya mkewe, Alicia
“Hello
wapendwa wangu. Ninaamini wengi wenu, kama sio wote, mnafahamu kwamba
Jumatatu Juni 4 nitafanyiwa operesheni ya mwisho kwenye mguu wa kulia,” amesema
“Ni operesheni
kubwa inayotazamiwa kuchukua takriban saa nane kwa taarifa nilizopewa tangu
mwanzoni mwa wiki hii. Hivyo madaktari wangu wametumia muda mrefu kidogo
kuniandaa kwa ajili ya Jumatatu.”
Ameongeza,
“Napenda niwajulishe kwamba ninajisikia vizuri kiafya na baada ya kuwa
kitandani tangu Aprili 11 (2018) nilipofanyiwa operesheni ya pili, sasa
niko tayari kwa ajili ya hii ya mwisho. Madaktari wangu wako vizuri. Nina imani
watafanya kazi nzuri ya kitabibu.”
Lissu
alishawashukuru wote waliomsaidia tangu aliposhambuliwa kwa risasi hadi sasa na
kuwataka wazidi kumuombea.
“Bado safari ni ndefu lakini ninaweza kusema
nimeanza kuona mwanga katika hili tanuru refu. Nimesema mara nyingi kwamba
ninaona fahari na faraja kwamba Watanzania wenzangu na wasio Watanzania
wamenitibu na wanaendelea kunitibu.
Najua
mtaniponya kwa nguvu za Mola wetu na kwa upendo na ukarimu wenu. Nawaombeni
msichoke. Nawashukuruni sana,” amesema.
Lissu kufanyiwa upasuaji wa 21
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment