Wapagazi
wanaopanda Mlima Kilimanjaro wamejitolea kuzoa taka za plastiki eneo la
Kwamrombo Jijini Arusha kwa lengo la kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
Wapagazi hao zaidi ya
100 wa kampuni ya utalii ya Easy Travel And Tours Ltd walijotolea kuokota chupa
za plastiki soko la Kwamrombo hadi eneo la Kona ya Mbauda Jijini Arusha.
Akishiriki katika
zoezi hilo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia alisema wapagazi
hao wameona umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuokota chupa za plastiki na
mifuko ya plastiki ili kuzichakata kwaajili ya kuzalisha mali ghafi.
Alisema kwakuwa eneo
hilo la kwamrombo ni maarufu kwa watu kula nyama hata takataka za plastiki
zinakuwa nyingi hivyo zoezi hilo ni zuri kwani hivi sasa wananchi watajua
umuhimu wa kutenga taka za plastiki kwaajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa
kampuni ya Easy Travel,Musadic Husein amesema wameamua kufanya usafi katika
eneo hilo kwaajili ya kutunza mazingira ikiwemo kuhakikisha taka za plastiki
zinachakatwa sambamba na kuzalisha bidhaa mbalimbali za majumbani ikiwemo mbao.
Naye mmoja kati ya
wafanyakazi hao,James Makoye amesema zoezi hilo liwe endelevu kwaajili ya
kusaidia Jiji la Arusha kuwa safi sambamba na wananchi kujengewa utamaduni wa
kuhakikisha wanatunza mazingira kwente maeneo yanayowazunguuka
Wapagazi Wajitolea kukusanya chupa za plastiki jiji la Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment