Mbunge wa Kaliua (CUF),
Magdalena Sakaya ameweka wazai kuwa yeye ndiye anayepaswa kuhojiwa
kuhusu matumizi ya Chama cha Wananchi (CUF) na si Katibu Mkuu, Maalim
Seif Sharif Hamad.
Sakaya
ametoa kauli hiyo leo bungeni Juni 5, 2018 wakati akichangia hoja ya
Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji aliyetaka Maalim Seif kuhojiwa
kwa kutokupeleka taarifa za CUF kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG).
“Maalim Seif toka mwaka 2016 hayuko ofisini. Mimi ndiye
najua matumizi ya CUF napaswa kuhojiwa. Suala la kusema Serikali imetoa
fedha, ruzuku imetolewa kwa CUF kama taasisi na Takukuru ije kunihoji
mimi na si Maalim Seif. "Huwezi kujua mambo ya ofisi kama hauko ofisini,
hawezi kujua mambo ya ofisini kama yuko mitaani,” amesema.
Awali Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji alivitaka vyombo vya
ulinzi na usalama kumhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
kwa kutokupeleka taarifa za matumizi za chama kwa Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Akichangia bajeti ya wizara ya fedha na mipango ya mwaka 2018/19 leo
bungeni Juni 5, 2018, Khatibu alisema kwamba Seif hajakitendea haki
Chama kwa kuacha kupeleka hesebu kwa CAG.
“Kama chama changu kimeshindwa kupeleka taarifa zake kwa
CAG kukaguliwa na kama hakijapeleka, Napata wapi ujasiri wa
kuhoji Sh1.5 trilioni?.
Sakaya amkingia kifua Maalim Seif bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment