Waziri wa Fedha na Mipango,
Dk Philip Mpango amesema ahadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kutoa
Sh50 milioni kila kijiji itaanza kutekelezwa mara baada ya mfumo wa
kuanza kuzitoa utakapokamilika.
Dk
Mpango ametoa kauli hiyo leo jioni bungeni wakati akijibu hoja ya
Mbunge wa Karagwe (CCM), Innocent Bashungwa aliyoitoa wakati Bunge
likiwa limekaa kama kamati kupitia vifungu kwa vifungu vya Bajeti ya
Wizara ya Fedha na Mipango ya mwaka 2018/19.
Bashungwa amesema, “Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020,
tulitoa ahadi ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji.” “Bajeti ya mwaka
2016/17 ilitengwa Sh60 bilioni na mwaka 2017/18 ilitenga Sh60 bilioni
lakini mpaka sasa hazijaenda, nataka kujua kwa nini hazijaenda?” Amehoji.
Akijibu hoja hiyo, Dk Mpango amesema, “ni kweli jambo hili ni ahadi
ya chama na ninaomba nikumbushe kwamba ni ahadi ya chama kwa kipindi cha
miaka mitano.
Serikali yafunguka Millioni 50 kila kijiji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment