Rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza anatarajiwa kuipokea Katiba mpya ambayo inaanza kutekelezwa
siku ya Alhamis ambayo inatajwa kuwa itageuza mambo mengi kwenye taifa
hilo, lakini pia kutoa fursa kwa Rais kuweza kuwania uongozi wa nchi
hadi mwaka wa 2034.
Ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Burundi kuwa na sherehe za kuipokea katiba mpya,wataalam wa siasa za Burundi wanahisi utaratibu huo mpya ni ujumbe wa Rais Nkurunziza kukamilisha malengo yake ya kuitawala nchi hiyo bila kikomo.
Katiba pia inaanza kutekelezwa wakati mazungumzo ya amani yakiwa yamekwama baada ya serikali kukata kuketi meza moja na wapinzani.
Rais kupokea Katiba Mpya Alhamis
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment