Jambazi
Sugu ambaye alikuwa anatafutwa kwa kufanya matukio ya Uhalifu hapa Jijini
Arusha Aliyefahamika kwa jina moja la Riziki mwenye umri kati ya Miaka 35 hadi
45 ameuwawa kwa kupigwa Risasi na Kikosi maalum baada ya majibizano ya Risasi
na Askari hao.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'azi amesema kuwa jambazi huyo ameuwawa tar 4 mwezi wa 6 katika eneo la Stendi ya Haisi Kilombero baada ya Polisi kupata taarifa za kintelijensia kuwa kuna Jambazi anayejihusisha na uhalifu wa unyanganyi kwa kutumia Silaha pamoja na wenzake wawili walikuwa waanapanga kuvamia kituo kimoja cha Kuuzia mafuta mjini hapa.
Amefafanua kuwa baada ya kupokea taarifa askari walipoenda Eneo la Tukio kwa lengo la kumkamata ,jambazi huo aliwaona askari na kutoa silaha yake aina ya Bastola na kuanza kurusha risasi kwa nia Ya kuwalenga askari wanaotaka kumkamata na kwa bahati mbaya risasi moja ilimjeruhi mguu wa kulia mpita njia aitwaye Halima Salim mwenye Umri wa Miaka 20.
Aidha baada ya tukio hilo polisi walilazimika kujibu mapigo na kupiga risasi moja ambayo ilimjeruhi sehemu ya Juu ya Tumbo jambazi huyo na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mount Meru ambapo alikutwa na silaha aina ya Chinese iliyofutwa namba ikiwa na Risasi ndani ya magazine.
Katika tukio jingine huko wilaya ya arumeru jana Tar 4 mwez wa 6 muda wa saa moja usiku katika eneo la Ngarasero kata ya Usariva mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume ambaye jina la halijafahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 hadi 30 alikutwa pembezo mwa barabara akiwa amefariki dunia huku mwili wake ukiwa na jeraha kichwani lilitokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali ambapo hadi sasa chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kuweza kubaini chanzo wahusika wa tukio hilo

Jambazi Sugu auwawa kwa Risasi na Polisi ,Huku Mpita njia akijeruhiwa kwa Risasi ya Mguuni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment