Mtuhumiwa wa ubakaji ambaye ni mwalimu aliruka ukuta wa shule na kukimbia baada ya kugundua taarifa za tukio hilo zimefika katika ofisi ya walimu na mama wa mwanafunzi huyo
Mwanafunzi huyo alichukuliwa na kukimbizwa katika kituo ch afya cha karibu na kupimwa ujauzito na maambukizi ya magonjwa ya zinaa bahati nzuri alikutwa yupo salama
“Tumeandika maelezo Polisi, ninachotaka ni haki kwa mwanangu, mwalimu aliyefanya hivyo akamatwe na kufikishwa mahakamani” amesema mama wa Binti
Akithibitisha tukio hilo mkuu wa Polisi katika eneo la Narumoru kamanda Job Lesikinwa amesema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kumtafuta mtuhumiwa wa tukio hilo.
Mwalimu abaka mwanafunzi na kukimbia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment