Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Joyce
Ndalichako aliwataka watanzania kuwaenzi pacha walioungana, Maria na Consolata
Mwakikuti kwa kujituma katika kazi
Akizungumza katika ibada ya kuaga miili ya
pacha hao waliofariki dunia katika hospitali ya mkoa wa Iringa, Juni 2, 2018,
Profesa Ndalichako amesema pacha hao wameifundisha jamii kuwa uvumilivu ni
silaha pekee katika maisha
Amesema jamii inapaswa kujenga utamaduni wa
kuwapenda na kuwaenzi watu wenye ulemavu na kutowafichwa kwa kuwa hakuna
anayeijua kesho
"Maria na Consolata mmelala hapo mbele
Mungu awape pumziko la milele, maisha yenu yamekuwa ushuhuda mkubwa
kwetu," amesisitiza
Profesa Ndalichako amesema hakuna haja ya
kutengeneza mafarakano kuanzia ngazi ya familia, "Maisha yao duniani
yamekuwa ya kujituma na ushuhuda mkubwa kwetu."
Kuhusu elimu yao, Profesa Ndalichako amesema
Serikali iliwapatia ruzuku na sio mkopo kama ilivyo kwa wanafunzi wengine
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Ikupa Alex amesema mambo mawili ya
kujifunza kutoka kwa pacha hao ni kutokata tamaa na kujiamini
“Walemavu wengi hawajiamini kwa sababu tangu
kwenye familia wameandaliwa mazingira ya kutojiamini, walemavu wenzangu
tujiamini," amesema ambaye pia aligusia miundombinu ya baadhi ya majengo
nchini kutokuwa rafiki kwa walemavu.
Profesa Ndalichako awataka Watanzania kuiga kujituma kwa Maria na Consolata
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment